Mapenzi ya Kweli
Kila mtu anamtafuta Mpenzi huyu
Unaweza Kupata Mapenzi ya kudumu
vitu unavyo tamani
awenavyo mpenzi wako!!!!!
By: Sadick Bakema
Kupata Mchumba Kamili:
Watu wengi wenye
sifa duniani hawajawahi kupata mapenzi ya kudumu. Kesi yako inaweza kuwa
tofauti.
Inaonekana kwamba ndani yetu kuna nafasi
kubwa ambayo haiwezi kujazwa na wachumba mia. Hata hivyo kuna tumaini. Ndoto
yako inaweza kutimizwa.
Thubutu kufikiri ya kwamba:-
Mwanamke anafaa kupendeza kiwango gani
kumfanya asitake upendo tena?
Naamini ni swali
gumu sana. Pengine linaweza kukupa wasiwasi wa kupenda. Mwanaume anahitaji
kuona wasichana wangapi uchi kabla
ya kujisikia kama anapendwa? Kila mtu ndani yetu analilia upendo! Sote
tunatafuta upendo, hakuna kitu kinachoweza kuchukua nafasi ya upendo.
Wanasayansi na madaktari wamethibitisha kwamba watu wanaofuata umalaya, na aina
za ngono zisizo kawaida huwa wanatafuta upendo wa kweli.
Umetoswa ndio sawa ndo unaamua kutopenda tena?
Watu wengi huamua kufanya uamuzi huo. Lakini
si kweli kwwani hata ukikaa miaka 20 bila mpenzi labda kwa dhana ya nisahau
maumivu. Je!! Ndio suluhisho la kuingia kwenye mikono mwema baada ya kuamua
kuwa na mpenzi? Jibu ni hapana. Kwani wakati ukiwa na chuki walikuja wenye
upendo wa kweli lakini ukawakataa, na sasa unaamua kupenda wamekuja wenye
upendo wa kubabaisha (Chapa ilale).
Ni kuwa makini na uchaguzi wakona kufanya
maamuzi sahihi ambayu baadaye huwezi jutia uamuzi wako. Ninaimani Website hii
inaweza kukupa uwezo wa kumtambua mpenzi wa kweli
Hata hivyo kupata upendo ni jambo tata. Sura
mzuri hunyauka. Mchumba hugeuka. Ndoa inaweza kuvunjika mkeo/mumeo akifa. Na uchungu utakaohisi huzidi
kama upendo kati yenyu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Lakini kama mlikuwa hampendani
faraja huingia. Nitaendelea kujitahidi kutoa ushauri wa kimapenzi ingawa
ninaamini wapo ambao huwa hawakubali ushauri kwa imani zao.
Ukweli
kwa wengi hutisha sana, lakini matarajio yetu huwa hazishikiki! Matakwa yetu ya
ndani kabisa huonekana kuwa mbali sana hadi sisi hujaribu kuvikana. Kana
usikane, kubali ukatae matarajio yetu hubaki ndani yetu.
Kwa muda mfupi tu, hebu tazama matarajio
yako...usijali ugumu wa kuzipokea. Angalia matarijio yako, ona vile yanakwambia
Unamtaka mtu ambaye:-
1.
Atafanya usikie kama umeheshimika
2.
Anakuamini na unamuamini
3.
Hamna siri kati yenyu
Kwa
ndani unatamani mtu mwenye:-
4.
Werevu, nguvu, uzuri usionyauka hata akizeeka
5.
Anajua yote ambayo umepitia maishani na kabla
hajawa na wewe
6.
Atakuelewa kabisa kila wakati Unaomtaka mpenzi
huyo
7.
Atatimiza mahitaji yako kikamili, yani ni kama
mliumbwa muwe pamoja
8.
Anasikia uchungu na wewe na anaweza kukusaidia
hata kuharibike vipi
9.
Anajuauovu wako, fikira zako na bado anakupenda
na anakuheshimu
Anaweza kuwa na wewe
mahali popote wakati unamhitaji
Atakupenda daima na
mapenzi kuu yenye kukufurahisha na kukutosheleza
Anakusaidia kila
wakati na kukuwezesha kufanya makuu Unahitaji mtu atakaye kusaidia kila wakati,
lakini anakupatia nafasi ya kukuwa kibinafsi; mtu ambaye hatakuchosha, na
ambaye hatawahi kugueka.
Mwishowe, liwe liwalo, unataka kuwa
huru kutokana na uwoga wa kumpoteza mpenzi wako. Unataka mpenzi ambaye hata
wahi kugonjeka, kulemaa au kufa.
Niliyokuandikia inaonekana kama
upumbavu!
Huyu Mpenzi mwenye urafiki usio na
kifani na nguvu bila mwisho ndiye anayeweza kujaza ufa ulio ndani yako. Huyu ndiye Mpenzi sote tunatafuta.
Kumwamini mtu
haimanishi mnapendana. Pia kumwamini Mungu hitiruhusu kuishi na Mungu. Kuenda
kanisani au Msikitini haitoshi. Ndoa
kamilifu hufanyika wakati mmeaminiana vikamilifu hadi unampa yote ulionayo na
yote uliyo. Mungu yu-tari kukupatia yote
alionayo na yote alio, lakini ili ndoa itendeke, lazima kuwe na makubaliano.
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments:
Thank you for you comment